Matthew 23:1-6

Isa Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo

(Marko 12:38-40; Luka 11:39-52; 20:45-47)

1 aKisha Isa akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake: 2 b“Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, 3 chivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 dWao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza.

5 e“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao. 6 fWanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi.
Copyright information for SwhKC